INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, December 6, 2012

SHILOLE AANGUA KILIO UKUMBINI......

MSANII wa filamu na Muziki wa kizazi kipya Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, usiku wa kuamkia Desemba 3, mwaka huu aliangua kilio mbele ya umati baada ya kukumbushwa misiba ya wasanii wenzake, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ na Steven Charles Kanumba.


Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiangua kilio baada ya kuwakumbuka wasanii wenzake Kanumba na Sharo. Tukio hilo lilitokea kwenye sherehe ya kutimiza miaka 13 ya Clouds FM, iliyofanyikia Club Bilicanas, Posta jijini Dar es Salaa.
Kilio cha Shilole kilisababishwa na Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu baada ya kutoa fursa ya kuwakumbuka wasanii maarufu waliotangulia mbele ya haki.


...Shilole akiwa na simanzi baada ya kuwakumbuka wasanii hao. Akiwa jukwaani Mchomvu aliwaomba mashabiki waliojazana ukumbini humo kunyanyua mikono juu na waliokuwa na simu aliwataka wazinyanyue juu huku wakiwa wameziwasha ili zitoe mwanga.
Mtangazaji huyo alianza kuyataja majina ya mastaa waliofariki mmoja baada ya mwingine, huku watu kibao wakionesha simanzi zao.


...Kilio kikiendelea. Alianza kulitaja jina la Steven Kanumba kisha Sharo Milionea, akifuatiwa na marehemu Complex, Vivian na wengine kibao, ndipo Shilole aliposhindwa kuvumilia na kuangua kilio kama mtoto kutokana na uchungu wa kuwapoteza wasanii hao.
Msanii huyo alianza kubembelezwa na wenzake aliokuwa amekaa nao karibu na baadaye kutulia.


Marehemu Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea'.

Marehemu Steven Kanumba.
 
Source: Vituko vya mtaa!

No comments:

Post a Comment