INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, February 4, 2016

Home Coming Na Going Bongo Ni Fundisho Kwa Watengeneza Filamu Tanzania: Rose Ndauka

Msanii wa filamu Rose Ndauka amesema kuwa filamu mpya ya Homecoming pamoja na Going Bongo ni filamu bora zaidi kuzinduliwa nchini mwaka 2016 ambapo amewataka wasanii wa Tanzania kuiga mfano.
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Rose alisema kila msanii wa filamu aliyoangalia filamu hizo lazima alitoka na kitu.
“Mwaka umeanza kwa changamoto ya kazi, hivi karibuni kuna kazi zilizinduliwa Homecoming na Going Bongo, ni kazi kali sana,” alisema Rose.

“Mimi binafsi nimezipenda sana, ni kazi zenye ubora, hata mimi zimenipa changamoto ya kujipanga zaidi. Kwahiyo mimi napenda kuwaambia wasanii wenzangu, hizi kazi ziwe ni fundisho kwetu mwaka huu, ukiangalia kwenye ubora wa picha, sound yaani safi kabisa,”
Rose ambaye pia alizindua magazine yake ‘Rozzie Magazine’ hivi karibuni, amewataka mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio wa filamu zake mpya zenye ubora.
Chanzo:Bongo5

No comments:

Post a Comment