INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, February 17, 2016

Producer Wa Mpango Mbaya Kwenda Nigeria Kuhudhuria Tuzo Za AMVCA 2016

MTAYARISHAJI na muongozaji wa filamu ambaye pia ni mwasisi wa Mtandao huu FC Staford Kihore anatarajia kutua nchini Nigeria kwa ajili ya kushuhudia utoaji wa tuzo za African Magic Views Choice Awards tuzo hizo ambazo zinatarajia kutolewa mwezi March 2016, akiongea na FC Kihore amesema kuwa anatarajia kutoa Lagos tarehe 2 March. 2016.

Mtayarishaji huyo ambaye pia ni muongozaji wa Tmt anakwenda kama mmoja ya watayarishaji wanaogombea tuzo huku yeye akipelekwa na filamu ya Mpango mbaya kazi bora kazi kutoka Swahilihood ikishirikisha wasanii nyota waliopikwa kutoka na mradi mkubwa kabisa wa Tanzania Movie Talent (TMT).
“Nitakuwepo kwa siku kadhaa nchini Naijeria kwa matukio makuu mawili au hata matatu kwanza kabisa ni kushudia utoaji wa tuzo nikishiriki kupitia filamu ya Mpango Mbaya, jambo la pili ni kuonana na kubadilishana mawazo na watengeneza filamu wakubwa kutoka sehemu mbalimbali za Afrika,”anasema Kihore.
Unapomuongelea Staford Kihore ana sifa ya kipekee kwani ndio Producer pekee aliyeweza kuwa mtayarishaji mkubwa wa filamu bila yeye kuwa mwigizaji kama historia ya watayarishaji wengi wa Swahilihood ambao wengi ni waigizaji mtayarishaji huyu amekuwa ndio mtayarishaji wa kwanza kutengeneza filamu za bajeti kubwa.
Tuzo za AMVCA-2016-
Tuzo za AMVCA-2016-
Na unapoongelea miradi mingi sana ya tasnia ya filamu Swahilihood hususani project za Filamucentral anahusika sana kama tuzo za BORA 2010, DAR FILAMU FESTIVAL (DFF 2013) ni mratibu na mwasisi pia sisi menejimenti ya FC tunajivuania mtu muhimu sana kwa maendeleo ya tasnia ya filamu Bongo.
Mwaka 2010 aliweza kutengenza filamu ya CPU kazi ambayo iliamsha ari kwa baadhi ya watengnezaji wa sinema kujiamini na kuazna kufuata nyayo zake kwani sinema hiyo iliweza kuonyeshwa katika majumba ya sinema na kushangiliwa sana na watazamaji, kila mara ukiongea Staford ni mtu anayependa mapinduzi katika tasnia ya filamu.
“Naweza kusema tasnia inapiga hatua na kila sehemu nayokwenda kwa safari za kikazi nafanya utafiti utakaoleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu na kuwa Industry kubwa Afika kila mtu awajibike alipo,”Kihore.
Ni matarajio yetu sisi kama wadau wakubwa wa tasnia ya filamu Swahilihood kuwa Kihore anapokkwenda Naijeria anarudi na ushindi mkubwa sambamba na tuzo FC inamtakia kila heri katika kupigania tasnia ya filamu.
Mpango Mbaya-Poster
source: FilamuCentral

No comments:

Post a Comment