INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, February 24, 2016

Shilole Amsaka Mwalimu Wa Kiingereza Ili Kumnoa Aonane Na Nicki Minaj.

Msanii Shilole au Shishi Baby, anatafuta mwalimu wa kumnoa kwenye lugha ya kingereza, ikiwa ni maandalizi ya kuonana na msanii wa Marekani Nicki Minaj.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Shilole amendika tangazo akimtaka mtu ambaye ni mwalimu wa lugha hiyo kuwasiliana, ili aweze kuanza mafunzo hayo.

“Anatafutwa mwalimu wa kingereza mzuri, jamani huu sio utani nipo sirias naona hali ishakuwa sio hali soon natakiwa kuonaa na Niki Minaji hivyo lazima nijinoeee, namba ya sm 0653883839”, aliandika Shilole kwenye ukurasa wake wa instagram
Shilole anafahamika kwa kutojua lugha ya kingereza, hivyo kuwa gumzo anapoongea lugha hiyo ambayo mara kwa mara huwa anachapia, lakini cha ajabu yeye mwenyewe huwa anafurahia na hajutii kuzungumza lugha hiyo ambayo haijui, kama alivyowahi kutamka neno la “I love is my country”, ambalo lilikuwa maarufu na watu kuvutiwa nalo.

1 comment: