INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, February 6, 2016

Masanja Mkandamizaji Kufungua Kituo Chake Cha TV Na Radio.

Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji ameweka wazi mpango wake wa kufungua kituo cha Radio na TV ambavyo atavisimamia yeye mwenyewe.
Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm Alhamisi hii, Masanja alisema tayari ameshapata mafunzo ya uandishi wa habari ili kujifunza kuhusu kuendesha vituo hivyo.

“Yeah nimepanga kufungua kituo changu cha radio na TV,” alisema Masanja.
“Nilikuwa na mpango wa muda mrefu ndio maana nikaenda shule ili kujifunza mambo mbalimbali kusuhu uendeshaji. Sasa hivi niko poa kabisa, najua vitu vingi hata nikiwaajiri watu hawata nidanganya kwa sababu najua kila kitu,”
Masanja licha ya kuwa ni muigizaji na mfanyabiashara, pia ni mkuliwa mkubwa wa zao la mpunga.

No comments:

Post a Comment