INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, July 3, 2016

Jokate Na Ali Kiba Wadaiwa Kurudiana.

Wapenzi mastaa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Alikiba Saleh ‘King Kiba’ wameombwa chondechonde na baadhi ya mashabiki wao kuwa sasa wafunge ndoa kwani penzi lao lina baraka ya Mungu kutokana na kukumbwa na migogoro lakini bado likaibuka kwa staili nyingine.

Jini Kabula Asweka Lupango.

Kibano! Staa wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amejikuta kwenye mikono ya sheria na kuswekwa lupango baada ya  kumtukana shosti yake, Miss Kinondoni 2009, Stella Mbuge.
Kwa mujibu wa mtoa ubuyu wetu makini, Kabula alitaitiwa na polisi usiku wa Jumatano iliyopita mara baada ya kutendo kosa hilo walipokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar wakitazama mechi kati ya Yanga na TP Mazembe ya DR Congo.

Abdu Kiba Asema Wasanii Wa Label Ya WCB Wanabebwa Na Promo.

Abdu Kiba amesema kuwa promotion ndiyo inawabeba wasanii wa lebo ya WCB.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, “Sijafikiria kuimba na msanii kutoka WCB,
kwa sababu sijaona anayeimba type ya muziki wangu.”
“Hata kama wana promote kwa sababu ndiyo walipoona wao ndiyo wanaweza wakafanya na watu wakaweza kuelewa lakini siku zote ajuae hazami,” alisema Abdu Kiba.
Aidha aliongeza kuwa bado hajaona msanii anayeimba type ya muziki wake ndani ya lebo hiyo [WCB].
Hata hivyo mapema mwezi huu msanii huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa yupo tayari kujiunga na lebo wa WCB kama watakubaliana na kuweka hela mezani kauli ambayo baadaye yeye mwenyewe aliipinga kuwa watu hawakumuelewa vizuri alichomaanisha.

Amanda Poshy Awachana Mastaa Wambwia Unga.

AMANDA Poshi, staa wa sinema za Kibongo, amewabwatukia baadhi ya mastaa wanaojitangaza kuwa wanatumia madawa ya kulevya baada ya kuathirika kuwa ni wanafiki.

Alisema angewaona wana hoja kama wangejitangaza kipindi walipoanza kuyatumia kuliko wakiona yanawashinda ndiyo wanakimbilia kwenye vyombo vya habari kuomba msaada.

Friday, June 3, 2016

Wema Alalama Kukosa Amani Sababu Ya Kuandamwa.

Msanii wa filamu na mjasiriamali Wema Sepetu amefunguka ya moyoni kutokana na namna mashabiki wake wa Instgram wanavyomchukulia na kumpa maneno ambayo muda mwingine yanamuumiza na kumkosesha amani na kumfanya ajione ni kama mkosaji mkubwa.

Rich Mavoko Asainishwa Rasmi Label Ya WCB

Msanii Diamond Platnumz, ameitambulisha rasmi label yake ya ‘WCB’ pamoja na kumsaini Rich Mavoko mbele ya waandishi wa habari.
Aidha, Diamond alimtambulisha dada yake, Queen Darleen kuwa mmoja kati ya wasanii wapya wa label hiyo.
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa, Godfrey Mngereza ambaye alizungumza na kumpongeza Diamond huku akiwataka wasanii wengine kushirikiana kwa namna hiyo.

Tuesday, May 31, 2016

Lazima Nimzalie Harmonize: Wolper

Jacqueline Wolper amenyanyua kinywa chake na kusema; “lazima nimzalie Harmonize (Rajabu Abdulhan, staa wa Bongo Fleva), kwa kuwa nimeridhika naye.”

Sijutii Kutembelea Bajaji: Wema Sepetu

STAA mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu amewafungukia wanaomsema vibaya kuwa siku hizi kafulia mpaka anatembelea usafiri aina ya Bajaj na kudai kuwa hayo ni maisha yake binafsi ambayo hayamhusu mtu yeyote.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Wema alisema kuwa anashangazwa sana na watu ambao wanafuatilia maisha yake kila kona kwa kuwa yeye ni binadamu kama walivyo wengine na maisha yote anastahili kuishi.

Sikumuimbia Jokate Wimbo Wa Aje: Ali Kiba

Alikiba amesema Aje si wimbo aliomuimbia Jokate wala msichana yeyote bali aliimba kwaajili ya mashabiki wake.
“Sijamuimbia mtu yeyote kwa kweli, mi nimeimba kwa ajili ya mashabiki wangu, kwanza sijawahi kumuimbia mtu kabisa, sijawahi, so ni kwa ajili ya mashabiki wangu,” Kiba alikiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV.

Picha: Harmonize Amtambulisha Wolper Kwa Wazazi Wake Huko Mtwara.

Ijumaa iliyopita Harmonize alikuwa Mtwara kwenye show, hata hivyo alitumia nafasi hiyo kwenda kumtambulisha mpenzi wake mpya Jacqueleine Wolper kwa wazazi wake. Angalia picha...

Wednesday, May 25, 2016

Aunty Ezekiel Aelezea Maumivu Aliyopata Wakati Wa Kujifungua Mtoto Wake Wa Kwanza.

Msanii wa filamu Aunt Ezekiel amefunguka na kueleza jinsi alivyopitia maumivu makali wakati wa kujifungua mtoto wake wa pekee ‘Cookie’ ambaye ametimiza moja mmoja hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa instagram, Aunt Ezekiel aliandika:

JB Azitolea Nje Ofa Za Filamu Za Kinageria, Ijue Sababu.

JB si msanii anayezuzuka na filamu za Kinaijeria ndio maana amesema ameshazitolea nje ofa tatu za kuigiza filamu za Kinaijeria.
“Natoboa siri ambayo watu hawaijui, nimekataa script zaidi ya tatu Nigeria kwenda kuact kwasababu hazinilipi,” muigizaji huyo aliiambia 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Martin Kadinda Azungumzia Ugomvi Wa Mirror Na Petit Man.

Martin Kadinda amefunguka juu ya ugomvi wa Mirror na Petiti Man. Akizungumza na Enewz Kadinda alisema kuwa ugomvi wa Mirror na Meneja wake anayesimamia kazi zake za muziki yaani Petit man ni utoto tu unawasumbua.

Sababu Ya Wolper Kumbwaga Mkongo Na Kuwa Na Harmonize Ni Hii Hapa.

Mwigizaji Jackline Wolper jana amefanya mahojiano na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha TakeOne na kuzungumzia mambo mengi kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake Putin ‘Mkongo’ aliyemvisha pete, na uhusiano wake na msanii Harmonize.
‘Ni kweli Raj (Harmonize) ni mpenzi wangu,ukweli nilimjua siku nyingi nilikuwa nikimchukulia kama mwanamuziki tu, tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa’’ alisema Jack.

Mimi Ni Zaidi Ya Ray: Gabo Zigamba

Msanii wa filamu nchini ambaye anafahamika kwa kuigiza kwa lafudhi ya Kimakonde Gambo Zigamba amefunguka na kusema kuwa yeye ni zaidi ya msanii Ray Kigosi kwenye kazi kwani yeye anafanya zaidi ya Ray.
Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz Gambo Zigamba aliweka wazi kuwa kipindi ambacho wakina Ray na wasanii wengine wakongwe wanafanya kazi zao hizo kulikuwa hakuna wasanii wengine wachanga ndiyo maana walikuwa wanaonekani ni wazuri sana lakini hivi sasa tasnia imekuwa na vipaji vipya ambavyo vinafanya vizuri zaidi yao hao wakongwe.

Ali Kiba Amuombea Kura Diamond BET Awards.

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kwa mafanikio aliyopata toka amerudi kwenye muziki tena ndani ya muda ni mfupi ni sawa na kuchana msamba kwake maana siyo hatua za kawaida.
Alikiba alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusisitiza kuwa yeye kusaini mkataba na kampuni ya ‘Sony Music’ jambo kubwa sana katika maisha yake ya muziki.
“Kiukweli toka nimerudi rasmi kwenye game na kutoa wimbo wa Mwana mashabiki walipokea vizuri sana Africa Mashariki, na kadili nilivyokuja kutoa wimbo mwingine wa Chekecha walizidi kuongezeka mashabiki na kujiona nina mashabiki wengi, hivyo kuja kusaini mkataba na ‘Sony Music’ ndani ya muda mfupi hivi kwangu mimi najiona ni kama nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida” alisema Alikiba.

Tuesday, May 24, 2016

Picha: Wema Sepetu Azindua Application Yake Ya Simu.

Jana Wema Sepetu Alizindua application yake ya simu kwa ajili ya kuwa karibu na amshabiki wake. uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na waziri wa sanaaa, utamaduni na michezo Nape Nnauye. Hizi ni picha toka kwenye event hiyo...

Friday, May 20, 2016

Zari Na Mama Diamond Watifuana ?

Inadaiwa ilitokea lakini haikuandikwa! Kuna habari kuwa, ile safari ya familia ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kula bata kwenye nchi za Ulaya, ilikuwa na mambo mengi lakini kubwa ni madai ya kuwepo kwa mtifuano kati ya mama Diamond, Sanura Kasim na Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenzake, Diamond.
Kwa mujibu wa chanzo, mtifuano kati ya Zari na mkwewe huyo ulitokea baada ya siku moja mkwe huyo kuteleza kwenye ngazi za umeme wakiwa wanapanda, Zari akamuwahi kwa kumshika mkono hali iliyomtibua mama huyo.

Rose Ndauka Aelezea Siri Ya Mafanikio Yake.

MKALI wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa siri ya mambo yake kumnyookea kuwa imetokana na kumuhusisha Mungu kwa kila anachokifanya na wala si vinginevyo kama watu wanavyodhania.
Akizungumza na Amani, Rose ambaye kwa sasa anamiliki kampuni inayojishughulisha na kutengeneza Jarida la Rozzie, alisema kuwa Mungu ndiye aliyemtendea miujiza hiyo kwani asingemshirikisha asingekuwa hapo alipo.

Wema Sepetu Amfungukia Ali Kiba.

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa msanii Alikiba ni mtu wa kumuacha kutokana na uwezo wake wa kuimba na namna ambavyo anaweza kuipangilia sauti yake kwenye muziki.
Wema Sepetu amezidi kuonyesha mapenzi aliyonayo kwenye kazi za msanii Alikiba na kusema huwa zinamkosha sana na kudai hajawahi kumuangusha siku zote