INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, March 7, 2015

BARNABA: WAIFU WANGU NI MODO MKALII!

MAMBO vipi msomaji wa safu hii ya Mpaka Home, tumekutana tena katika maeneo yetu ya kujidai. Ni sehemu pekee ya kuweza kujua maisha halisi ya mastaa nyumbani kwa mastaa wetu Bongo.


Barnaba akiwa na mke wake.

Wiki hii nimetia timu mitaa ya Mwananyamala-Komakoma, kumsaka kijana machachari, anayesumbua kwa kuwa na sauti kali ya kumtoa nyoka pangoni, si mwingine bali ni Barnaba Elias.
Nyumbani kwake Barnaba anaishi na mkewe halali wa ndoa, Zubeda Mussa, pamoja na mtoto wao kipenzi, Steve.Amezungumza mengi, twende pamoja:

RATIBA YAKE YA SIKU IKOJE?
“Mimi naamka mapema sana saa 11:00 alfajiri kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kukimbia, baada ya kurudi mazoezini, naoga kisha napata kifungua kinywa halafu narudi tena kulala kwani ninakuwa nimeamka mapema sana na kama sina kazi siku hiyo nitaamka mchana na kufanya kazi zangu kwenye studio yangu ambayo nimeifungua hapa nyumbani inayoitwa High Table Sound.”


Barnaba Elias akiwa na familia yake.

ANAPENDA KUFANYA NINI AKIWA NYUMBANI?
“Kwa kweli hakuna kitu nachokipenda zaidi kama kukaa na familia yangu, kujadili zaidi maisha mimi na mke wangu na mara nyingi napenda kucheza mpira na mwanangu kitu ambacho tunakifurahia wote.”

ANAPENDELEA CHAKULA GANI?
“Kwa upande wa chakula, napenda sana ugali, wali, ndizi na mbogamboga kwa upande wa mchana lakini kifungua kinywa nakunywa chai na kitu chochote aina ya mkate kwa ajili ya sauti.”

NI WAGENI GANI ANAWAHITAJI KWAKE?
“Mimi napendelea sana wageni wastaarabu na wenye heshima ingawaje sichagui mgeni wa kuja kwangu kwa sababu napenda sana wageni.”

Mwanamuziki Barnaba akiwa kwenye studio yake ya nyumbni.

NINI AMBACHO ANAKITAMANI KWA SASA?
“Unajua kwa sasa nina mtoto wa kiume lakini natamani sana mtoto wa kike angekuwepo hapa nyumbani ingekuwa poa sana lakini naamini Mungu atanipa tu.”

KUNA TOFAUTI ALIVYOKUWA KWAKE NA KWAO?
“Tofauti ni kubwa sana kwa kweli, kule nilikuwa chini ya wazazi wangu lakini hapa na mimi ni baba wa familia na ninajipangia mimi mwenyewe vitu vyangu na familia yangu.”

ATAENDELEA KUISHI KWENYE NYUMBA YA KUPANGA?
“Kwa kweli Mungu akinisaidia mwaka huu na mimi nitakuwa nimeshahamia kwangu, nashukuru nimejitahidi na mimi nimepata kwangu sasa.”VIPI UNAMSHIRIKISHA WAIFU KWENYE MUZIKI WAKO?
“Ndiyo kama katika wimbo wa Wahaladee, nilikuwa sioni haja ya kumtafuta Video Queen (modo) mwingine wakati mke wangu ana vigezo vyote, ni mkali ambapo nilimuweka na akafiti kwelikweli.”

No comments:

Post a Comment