INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, March 6, 2015

MTANGAZAJI WA TIMES FM APORWA iPHONE 6 ZENYE THAMANI YA MILIONI 3.8

Mtangazaji wa kipindi cha The Switch cha Times FM, Cnda King ameporwa simu ya thamani kubwa ya iPhone 6 yenye dhahabu (24 karat gold plate).


Cnda ambaye pia ataanza kuonekana kwenye kipindi kipya cha TV kiitwacho 10 Made in Africa, ameimbia Bongo5 kuwa simu hiyo iliporwa jana Jumapili (March 1) akiwa kwenye taa za traffic maeneo ya Kamata, Kariakoo wakati akitokea airport mida ya saa mbili na nusu usiku.

iPhone 6 iliyozungushiwa dhahabu

“Nilikuwa kwenye mataa nasubiri taa ziruhusu magari kwenda huku nikichat,” amesema Cnda. “Kioo kilikuwa chini, akatokea jamaa na kunipora na kukimbia,” ameongeza mtangazaji huyo.
Cnda amesema gharama ya simu hiyo ukijumlisha na dhahabu zilizowekwa nyuma ya simu hiyo ni shilingi milioni 3.8.
“Niliinunua November last year ikiwa kawaida ila niliipeleka Hong Kong February mwaka huu ikawe pimped na hiyo 24 karat gold plate.”
Cnda hajaacha kuwaonya watumiaji wa simu kuepuka kuchat wakiwa kwenye foleni hasa katika maeneo yenye watu wengi.
“Watu wawe makini sana na hawa jamaa barabarani,” amesisitiza.
“Ukiacha kukuibia wanaweza kukuumiza pia.”

Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment