INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, March 2, 2015

MUME:SIKUBALI NDOA YANGU NA JACK IVUNJIKE!

Mwandishi Wetu/ijumaawikienda
MUME wa mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’, Gadna Dibibi amefunguka kuwa kamwe hawezi kukubali ndoa yake ivunjike kirahisi, atapambana hadi dakika ya mwisho.Kauli hiyo ya Gadna ameitoa ikiwa ni siku chache tangu vyombo vya habari viripoti kuwa wawili hao waliooana mwaka 2013, wamemwagana na kila mtu anaishi kivyake.


Mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’, akiwa na mumewe Gadna Dibibi.

“Sijampa talaka Jack hivyo bado ataendelea kuwa mke wangu halali, nitahakikisha hilo linabaki kuwa hivyo. Kama kupishana kauli, tulipishana na ni vitu vya kawaida lakini haiwezi kuwa ndiyo mwisho wa uhusiano wetu labda ningekuwa nimempa talaka,” alisema Gadna.Alipotafutwa Jack ili kusikia kauli yake kuhusu ishu hiyo, alisema: “Sitaki kuzungumzia hilo nipe muda kidogo.”

No comments:

Post a Comment