INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, September 20, 2015

Kijue Kilichomfanya Riyama Ally Kuishia Kidato Cha Pili.

Staa wa Filamu Bongo, Riyama Ally ameweka wazi kuwa hakumaliza elimu ya sekondari kutokana na ugumu wa masomo kwani hakuwa akiambulia chochote darasani licha ya walimu kujitahidi kufundisha kwa kiwango cha juu.

Akizungumza na Ijumaa  hivi karibuni, Riyama alisema kuwa kutokana na umbumbumbu wake alilazimika kuishia kidato cha pili baada ya masomo kuzidi kuwa magumu.
“Kwa kweli ugumu wa masomo ulinifanya niache shule, niliona kama wazazi wanapoteza pesa yao bure, sikuwa naambulia chochote, walimu walikuwa wakijitahidi sana lakini sikuwa naelewa kitu, kwa hiyo nimekomea kidato cha pili, masomo magumu asikuambie mtu,” alisema Riyama.
Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment