INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, September 17, 2015

Ray Asema Ushindani Kwenye Filamu Hakuna Baada Ya Kifo Cha Kanumba.

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’ amesema baada ya kufariki Steven Kanumba tasnia ya filamu imekosa ushindani wa ndani na nje.
Akizungumza kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Ray alisema kazi yake na maisha yake vimetikisika kutokana na kukosa mshindani kama alivyokuwa Kanumba.

“Kwa upande wangu vitu vingi vimetikisika kwa sababu Kanumba ndio alikuwa mshindani wangu, kwenye maisha yangu ya kawaida na filamu,” alisema.
“Kanumba alikuwa akifanya hivi lazima na mimi nijitahidi kufanya kingine. Mimi nimeenda Singapore kuchukua vifaa, yeye ataenda Marekani, huo unakuwa ni wivu wa maendeleo, baada kuwa unarudi nyuma unakwenda mbele. Sasa nilichoathirika kikubwa ni kukosa ule ushindani wa nje, ilifika wakati huwezi kumtaja Kanumba bila kumtaja Ray.”
“Nimeathirika sana kwa sababu hakuna challenge, ndio maana nasema kweli kuondoka kwa Kanumba kumeondoka na tasnia, yaani Kanumba alivyofariki sasa ule ushindani wa mimi na yeye ukawa tena haupo.”
Bongo 5

No comments:

Post a Comment