INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, September 27, 2015

Wema Sepetu Amtaja mwanaume Atakayeanzisha Nae Familia, Asema Hana Uswahili Kama Kina ......

BAADA ya kupita ukimya mrefu bila kuzungumzia mapenzi, mrembo asiyepoteza ubora wake, Wema Sepetu ‘Madam’ amemtaja mwanaume anayetarajia kumzalia mtoto kuwa ni Luis Munana, raia wa Namibia.
Wema alifunguka hayo juzikati mara baada ya mwandishi wetu kutaka kujua ana mpango gani kwenye ulimwengu wa ‘malovee’ ndipo alipomwanika Luis kuwa ndiye mwanaume pekee ambaye ameshafikia hatua ya kumuamini na yuko tayari kuzaa naye kwa namna yoyote licha ya kujua ana tatizo la uzazi.

“Luis ndiyo kila kitu kwangu, ndiye mwanaume ambaye tunaelewana na siyo mswahili kama kina mwafulani. Luis nitazaa naye hata kwa ku-adopt (kuasili) mtoto kama njia za kawaida zitashindikana, ndiye mwanaume ambaye nimepanga aje kuwa baba wa watoto wangu,” alisema Wema
Kabla ya kufunguka hayo, Wema alikuwa akimposti  mwanaume huyo ambaye alishiriki Shindano la Big Brother-Hotshorts (2014) kwenye ukurasa wake wa Instagram pasipo kuandika kama ni mpenzi wake lakini kwa sasa ameamua kuweka kila kitu hadharani.
Miezi kadhaa iliyopita, Wema aliwahi kuonekana na Luis katika pati ya Instagram iliyofanyika kwenye Viwanja vya Posta jijini Dar kisha wawili hao kudaiwa kulala pamoja katika hoteli moja jijini humo.
Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment