INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, December 27, 2015

Riyama Ally Na Flora Mvungi Wakabana Koo Kukata Nyonga.

STAA wa filamu Bongo, Flora Mvungi na shostito wake, Riyama Ally juzikati walijikuta wakigeuka kivutio ukumbini baada ya kufunikana kwa kuzikata nyonga bila aibu kwenye hafla ya kumpongeza mtoto wa Flora, Tanzanite Hamis kuchaguliwa kuwa balozi wa duka la kuuza nguo.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni Hoteli ya City Style Sinza-Mugabe jijini Dar es Salaam, ambapo wawili hao walivamia katikati ya ukumbi na kuanza kushindana kuzungusha nyonga hadi kufikia hatua ya kuacha kucheza wakiwa wamesimama na kuamua kulala chini.
“Jamani huyu si Riyama na yule aliyelala ni Flora, mhhh wanajua kuzikata,” ilisikika sauti ya mhudhuriaji ukumbini hapo.
Chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment