INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, December 22, 2015

Wasanii Tufanye Na Biashara Nyingine Tujikwamue Kiuchumi: Ire Uwoya

MKALI wa filamu nchini, Irene Uwoya, amewataka wasanii wenzake hasa wanawake kujituma katika kazi nyingine kama vile biashara ili kuweza kujikomboa kiuchumi
Irene amesema wasanii wengi wanategemea sanaa ili kuweza kuendesha maisha yao, lakini wanatakiwa kufanya mambo mengi ili kuweza kujiingizia kipato.

Akizungumza na MTANZANIA jana alisema yeye ana ofisi ambayo inajishughulisha na ushonaji wa nguo za aina zote ambayo inamsaidia kuingiza kipato na huwa anashona.
“Natumia kauli mbiu ya hapa kazi tu kwani mtu huwezi ukategemea kitu kimoja na hasa sisi wasanii huwezi ukategemea sanaa lazima utafute kitu kingine ambacho kitaweza kukusaidia,” alisema.
Alisema ni vema mtu akajiongeza katika kazi yenye uhalali ili aweze kufanya vitu vya msingi ambavyo vitamfanya kuendesha maisha yake.

No comments:

Post a Comment