INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, October 18, 2012

ODAMA SASA AINGIA KIKAZI ZAAIDI
MWANADADA nguli katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Jenifer Kyaka Odama ameingia katika kundi la akina dada wajasiriamali baada ya kuamua kufungua kampuni yake ya utengenezaji wa filamu kwa ajili ya utayarishaji wa filamu zake.

Kwa sasa hali ya ushindani ni kubwa sana kwa hiyo kama huna kampuni kwa ajili ya utayarishaji wa filamu zako utasumbuka hata kuharibu kazi yako.

Unapotumia kampuni ya nje unakutana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa kazi zako lakini pia unakosa usimamizi wa kazi hiyo, unaweza kupoteza muda kwani unapompatia kazi mtendaji hata kama ana kazi nyingi hasemi, hali ambayo huharibu ratiba kwa kucheleweshewa kazi hata kuharibiwa, anasema Odama.

Odama analia na wale wahariri wasio waaminifu kwani wao huwa ni sababu ya filamu kuchelewa au kuharibika, jambo ambalo linawakabili wasanii wengi kupoteza muda wa kutoa filamu zao kwa wakati.

Msanii huyo ni kati ya wasanii waliopo katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu sasa na ameigiza filamu 36.

Kati ya filamu hizo, filamu 9 ameshiriki akiwa kama mtayarishaji. Ameigiza filamu kama All About Love, Odama, Shumileta, Rude na filamu nyingine nyingi.Chanzo : Mwanaspoti
Written by Sports | February 21, 2012 | 0
Imechukuliwa kutoka katika tovuti hii: http://www.dullonet.com/sports/2012/02/21/odama-sasa-aingia-kikazi-zaidi/

No comments:

Post a Comment