INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, October 23, 2012

MSANII WA BONGO MOVIE 'MIRIAM' AKATAA KUOLEWA BAADA YA WAZAZI KULA MAALI




MSANII chipukizi kwenye tasnia ya filamu bongo, Miriam, ambaye ni mdogo wa msanii Jackine Wolper, amesema kuwa yupo kwenye wakati mgumu kwani wazazi wake wanamtaka aolewe kilazima na mtu ambaye hana mahusiano naye huku wakiwa tayari wameshachukua mahari.

Ishu hiyo awali kabisa ilidaiwa kuwa mwanaume ambaye amewekwa kwa ajili ya kumuoa ni mume wa mtu huku ndugu zake wakiwa wameshapokea nusu ya mahari tangu mwaka jana.

Mwandishi wa habari hizi, alimtafuta msanii huyo ili kuzungumza naye kwa kina juu ya hiyo, ndipo alipodai kuwa hawezi kusema lolote kwani haitaji kuolewa kwa sasa na kitu kikubwa kinachomtatiza ni kwamba mwanaume huyo tayari ni mume wa mtu.

Alidai baadhi ya ndugu zake wanadai kuwa nusu ya mahari imeshatolewa kwa ajili yake na endapo akikataa kufanya wanavyotaka hali itakuwa ngumu kwani hakuna kitu wanachoweza kurudisha kwa mwanaume huyo zaidi ya yeye kukubali kuolewa.

“Mimi siwezi kwa sababu sina mpango wa kuolewa kwa sasa lakini wazazi ndo kwanza wanataka mimi nifanye hivyo yani nashindwa kuelewa nifanye nini kwa hili, kila ndugu ninayemfuata kumbe anajua kila kitu juu ya hilo suala na walishindwa kunishirikisha mimi ili nitoe mawazo yangu,” alisema kwa unyonge.

No comments:

Post a Comment