INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, May 5, 2012


HAPATAKALIKI  UWANJA WA TAIFA,  TIMU YA BONGO MOVIE NA TWIGA STARS KUCHUANA LEO

Wachezaji wa timu ya Bongo Movie ambao baadhi yao leo wataingia uwanjani (picha na Maktaba)


Mechi maalumu ya hisani kwa ajili ya kuchangia timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars), kati ya timu hiyo na wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie sasa itachezwa leo (Mei 5 mwaka huu).

Kwa mujibu wa kampuni ya Edge Entertainment iliyoandaa mechi hiyo, imerudishwa nyuma kwa siku moja kupisha mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumapili.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni ambapo viingilio kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ni sh. 2,000, VIP C na B itakuwa sh. 5,000 wakati VIP A ni sh. 10,000.

Twiga Stars ambayo kwa sasa haina mdhamini na kambini katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani kujiandaa kwa mechi ya mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia.

Timu hizo zitapambana Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa na kurudiana Juni 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshindi atashiriki fainali za AWC zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment