INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, May 21, 2012


SHUJAA FLAVIANA MATATA AGAWA MABOYA 500 YA KUJIOKOLEA MAJINI, KATIKA KUMBUKUMBU YA KUZAMA KWA MELI YA MV BUKOBA

MAMA YAKE NAYE ALIKUMBWA NA KUFARIKI NA MV BUKOBA

Flaviana Matata alishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya meli ya MV Bukoba alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo yaliyopo Igoma jijini Mwanza, katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza mama yake mzazi. 

Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori kulia ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service,Kapten Obadia Nkongoki. Igoma jijini Mwanza,


Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo

Flaviana na wageni wakiweka  mashada kwenye makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo Igoma Mwanza

No comments:

Post a Comment