INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, May 7, 2012


WAKILI WA SERIKALI ADAI UMRI SAHIHI WA LULU UCHUNGUZWE

Kamera zikimfuata kwa shauku.
Lulu (katikati) akiingia mahakamani na askari magereza wa kike.
Hapa ni karibu na mlango wa kuingia katika chumba 
-----------
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi ametupilia mbali ombi la Mawakili watatu wanao mtetea a Muigizaji nyota wa Filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu (17) anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba, aliye fariki dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Vatican Sinza Jijini Dar es Salaam.
Mawakili hao wanao mtete Lulu ni Keneth Fungamtama, Fulgence Massawe, Peter Kibatala na Jackline De Meero.

Wakili Fungamtama alidai Mahakamani hapo kwamba kutokana na umri mdogo wa mtuhumiwa wanaiomba Mahakama itoe udhuru kwa mtuhumiwa Elizabeth kushitakiwa katika Mahakama ya watoto kwa kuwa ana umri chini ya miaka 18 pia kesi yake iwe INCAMERA.

Naye Wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda alidai Mahakamani hapo kwamba hawakubaliani na ombi hilo hivyo wanaomba wachunguze umri sahihi wa Elizabeth kwa upande wao ili ukweli uweze kubainika.

Kaganda alidai Mahakamani hapo kuwa umri wa Elizabeth unatatanisha kutokana na maelezo yanayotofautiana ya mtuhumiwa huyo alyoyatoa awali kwani alipohojiwa na Jeshi la Polisi alidai kuwa na umri wa miaka 17, pia majina yake katika cheti cha kuzaliwa ni Diana Elizabeth tofauti na linavyoandikwa katika kuwa Elizabeth Michael, upelelezi juu ya umri sahihi ni lazima.

Lulu amepandishwa kizimbani leo ikiwa ni mara ya tatu sasa ,mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam Augustina Mmbando, Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo na amerudhishwa rumande.

Hakimu Mmbando alitupilia mbali ombi hilo kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 196 kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai hivyo ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Tofauti na hali ilivyokuwa marambili ambapo mtuhumiwa Lulu alipoletwa Mahakamani hapo ambapo watu walijazana na kuvuta hisia za wengi jana hakukuwa na mikiki ya aina yeyote ile hivyo lulu aliweza kuonekana bila taabu huku wanahabari wakiweza kufanya kazi kama kumpiga picha bila taabu yeyote bila kuzuiwa na Askari Magereza wala kukanyagana.

No comments:

Post a Comment