INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, May 4, 2012

TUNASHUKURU BONGO FLAVA KWA KUONYESHA MAPENZI MEMA KWA NDUGU YETU SAJUKI KWA KUTUNGA WIMBO WA "MBONI YANGU" ILI KUMTIA MOYO NA KUHAMASISHA WATANZANIA KUMCHANGIA NDUGU YETU.



Nilisema nitakwambia kwa nini wimbo huu unaitwa MBONI YANGU.Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake.Kabla sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.Wimbo tuliokuwa tunaurekodi unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu tumeurekodi kuhamasishana kuchangia na utaanza kusikika kesho hapa clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.Na kesho tutahakikisha tunakusanya angalau Tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm.Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.

Sehemu ya pili ya picha katika utengenezaji wa wimbo mboni yangu.
Madee akipitia mashairi yake.
Kimodo na Barnaba
Ditto
Madee akirekodi sauti
Ditto,Amini na Afande Sele
Zamu ya Amini
Peter Msechu
Profesa Jay akiandika mistari yake
Afande Sele nae akiandaa mistari yake
Fid Q hakubaki nyuma
Wimbo huu tuliurecord mpaka mishale ya saa tisa kasoro usiku,nilikuwa nasinzia ila mapema saa kumi nambili leo alfajiri nilikuwa macho tayari.

Thanks kwa coordinator Ruge Mutahaba & Dina Marios
Director Mwasiti Almasi
Producer Tuddy Thomas

No comments:

Post a Comment