INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, May 13, 2012


KAENI MKAO WA KULA KITU KIKO MAKAANGONI KINAPIKWA- QUEEN SPEAR (AUNT FIFI)

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchiniTumaini Bigilimana ‘Aunt Fifi, anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Queen Spear, imefahamika. Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Aunt Fifi alisema kuwa tayari kazi ya uhariri imeshakamilika hivyo ameanza mchakato wa kuiingiza sokoni. Alisema anaamini mashabiki wa filamu wataipenda kazi hiyo iliyozingatia mila na desturi za Kitanzania kutokana na kukamilika kila idara kuanzia hadithi, upigaji picha, hadi washiriki waliohusika. Fifi ambaye ni mahiri katika utunzi wa filamu za kibongo huku akijaaliwa pia kuzitendea haki kazi zake alisema kuwa mwaka huu amepania kutayarisha filamu bomba zaidi ili kuweza kuwapa burudani zaidi mashabiki wa bongo Muvi. Aidha, Fifi ambaye ndiye mtunzi wa filamu ya Senior bachelor filamu iliyomletea tuzo kadhaa msanii Jacob Stephen ‘JB’ kupitia filamu hiyo ambayo, pia alipata kutayarisha filamu yake ya aliyoipa jina la Kizungumkuti na kufanya vizuri. Kama hiyo haitoshi Fifi alipata kutamba katika filamu mbalimbali zikiwemo Copy, Sound of Death, Senior Bachelor, I Deserve It, Kaburi la Mapenzi, Fake Smile, Daddy, Cross My Sin na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment