INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, February 18, 2015

HUYU NDIYE MNENGUAJI WA BENDI YA EXTRA BONGO ALIYEPIGWA NDOA VALENTINE DAYMnenguaji mkongwe wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ Otilia Boniface siku ya harusi yake.

MNENGUAJI mkongwe wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ Otilia Boniface siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ alipigwa pingu ya maisha na mchumba wake wa muda mrefu, Ally Kinde.

Ndoa hiyo iliyofungwa usiku nyumbani kwao Mbezi-Juu ilisindikizwa na ngoma pamoja na matarumbeta ambapo mitaa hiyo na ile ya Kinondoni nyumbani kwa bwana harusi ilisimamisha shughuli zote kwani wanawake waalikwa walijiachia kwa kukata mauno ya kufa mtu kihasara hasara.

Katika hali ya kushangaza, mwanaume mmoja aliyeonekana siyo riziki, aliwashtua watu baada ya kuonekana akikata mauno akiwa juu ya gari la Bwana harusi, jambo lililosababisha kutimuliwa na waalikwa.
Bwana harusi baada ya kufunga ndoa msikitini alikwenda kumpa mkono mkewe aliyekuwa ndani akimsubiri, huko alipokelewa kwa shangwe na wanawake waliokuwa wakibinuka isivyo kawaida.Otilia mwenyewe alikuwa na furaha muda wote huku akisema anamshukuru Mungu kufunga ndoa kwani ni miaka mingi imepita tangu alipovishwa pete ya uchumba. “Dah, siamini maana nimetoka mbali sana na nilisubiri kwa muda mrefu sana siku hii na kweli imetimia, namshukuru Mungu kwa kweli maana ni kwa neema tu,” alisema.

Gazeti hili lilizungumza na Bwana harusi na kumuuliza kwa nini alichagua kufunga ndoa Siku ya Wapendanao;
“Nimeamua kufunga ndoa leo maana ndiyo bethidei yangu, nikaona ni vema nikamchukua na nimpendaye ili iwe siku ya historia zaidi.”

dondoo: Flora aseme ukweli, ujomba wa yeye na Gwajima umetoka wapi? Hilo tu ndiyo nataka alifafanue kwa undani maana wajomba...

No comments:

Post a Comment