INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, February 21, 2015

MISS DODOMA AOKOKA

Stori: Shani ramadhani
Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans amemrudia Mungu kwa maana ya kuokoka kwa kile alichodai kutotimia kwa malengo aliyojiwekea.Akizungumza na mwanahabari wetu, Eva alisema tangu akiwa mdogo, alijiwekea kiapo kuwa endapo atashindwa kumpata mume mwema, basi atafanya kazi ya kumtumikia Mungu.


Aliyekuwa Miss Dodoma mwaka 2005, Eva Evans akiwa kanisani.

“Nakumbuka mapito yangu yote tangu nikiwa mdogo mpaka nikaingia kwenye masuala ya urembo nilijiwekea nadhiri ikifika muda mambo yangu hayajakamilika, itanibidi nimrudie Mungu wangu.

“Baada ya kupitia urembo nilichumbiwa, hapohapo nikaanza kuhudhuria mikutano mbalimbali ya neno la Mungu, siku moja Nabii akitoa neno, nilimsikia akisema kuna binti mmoja hapa anataka kuolewa apite mbele haraka sana, basi nikapita mbele na nilipofika pale alianza kuniombea na baadaye alianza kuniuliza maswali.


“Akaniambia mwanaume anayetaka kunioa hana sifa za kuwa mume bora na kama nabisha nimchunguze, basi nikamchunguza na kugundua kuwa hakuwa na sifa.“Basi nilivyojua tu nikaamua nisitishe mipango ya ndoa zikiwa zimesalia wiki mbili tu ili ndoa ifungwe, nashukuru Mungu nilieleweka, na kuanzia hapo nikaamua kuokoka kabisa, ninaomba sana Mwenyezi Mungu aniletee mume mwema,” alisema mrembo huyo. Eva alifunguka kuwa katika mashindano ya urembo kuna uchafu mwingi hivyo akawashauri wasichana walioko huko kumrudia Mungu.

No comments:

Post a Comment