INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, February 19, 2015

SIMULIZI YA NATASHA - 6




ILIPOISHIA
Wiki iliyopita tuliishia pale nilipoeleza kwamba nilishangazwa na kitendo cha kuona wanawake wengi wanavaa nguo nyeusi nchini Angola…ENDELEA
NiLIambiwa waliokuwa wanavaa vile walifiwa na  waume zao vitani.
“Mungu wangu mbona wengi!” nilishtuka.Katika kundi la wanawake kumi, saba wote wamefiwa!
Kingine niliona vijana wengi wakiwa wamekatwa ama miguu ama mikono!  Kuuliza kisa eti ni vita! Kumbe vijana wakifika miaka 18 ni lazima kwenda vitani, baada ya miaka miwili anarudi kilema (siyo wote wanaorudi vilema).
Utawaonea huruma siku yao ya matibabu, makundi ya vijana kumi hadi ishirini kila baada ya muda utaona yanapita wote wamekatwa kiungo kimoja au viwili. Wenye bahati zao wanarudi salama na kumshukuru Mungu.
Mdogo wangu Tony aliingizwa shule inayoendeshwa na Wafaransa, Alliance Francaise ndiyo ilikuwa shule pekee inayofundisha Kiingereza. Kwa hapo haikuwa mbali na nyumbani, mimi nikapatiwa kazi ubalozini ya usafi ambayo niliifurahia sana, kazi ni kazi nitake kazi ya maana nimesoma?
Kazi yenyewe hiyo kwanza ilikuwa kama hisani toka kwa mheshimiwa Balozi, ama sivyo angeuchuna tu.
Cherrie akabaki nyumbani na mama akimfanyia fujo. Neno la kwanza la Kireno kujifunza likawa ni embaixada, nilihisia tu hata kabla sijauliza kuwa maana yake ni embassy kwa maana ya ubalozi, nikaambiwa sawa nimepatia.
Likaja la pili, bondia nikataka kujibu mimi siyo Mohamed Ally lakini ukiwa nchi ya watu usijifanye kimbelembele kujibu vitu maana kila eneo lina namna yake ya kuzungumza, mfano umetoka juani na kiu imekushika ukafika kwa Muangola anaweza akakuuliza akupe sumu?

Kibongo lazima utakataa hakuna mtu anayependa kufa siyo? Lakini kiukweli utashangaa sana ukiona wenzako wanapewa kinywaji na wewe mate yanakutoka kwa kunyimwa, kumbe sumu kwa Kireno ni juisi!
Meza ni meza. Kinyentu (nimeandika kwa Kiswahili) ni sh. mia tano wakati huku masela wanasema nyentu ni mia. Barida kule inatamkwa bariga maana yake tumbo. Fala si kwamba anakudharau ila maana yake sema! Huku kona ni kona kule ni neno lisiloweza kutamkika hadharani.
Shega kule maana yake inatosha, kuna maneno mengine yanafanana na Kiingereza hivyo unaweza kuhisi ni neno fulani ila hili la bondia ilibidi niwe mpole kuuliza maana yake ni nini? Kumbe Habari ya asubuhi! Upo hapo?
Kwa vile nilikuwa nikifanya kazi na pia kuna wafanyakazi wengine kama vile dereva Sumai, baba mtu mzima mwenye asili ya Kongo lakini kalowea Angola, nilifahamu Kireno haraka.
Kitu cha kuchekesha wananchi wa kule siyo wengi wanaofahamu Kiingereza ila usiwatete kwa Kiswahili, tulipoligundua hilo tukawa tunaogopa kuongea hata Kiswahili njiani maana ghafla anaibuka mtu akikusapoti unachoongea na kukwambia alikulia Morogoro au Dar, sasa ole wako uwe umemteta!
Kutokana na cheo cha baba, alikuwa akipokea vijana wageni waliojitosa kwenye kazi ya ubaharia.

No comments:

Post a Comment