INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, February 26, 2015

MAMA DIAMOND AREJEA KUTOKA INDIA, YUPO FITI

Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama yake Sanura Kassim.

MUSA MATEJA/Amani

HAKUNA neno linaloweza kusemwa kwa mara nyingine zaidi ya Mungu ni mwema! Kauli hiyo inakuja kwa mara nyingine baada ya mama mzazi wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim a.k.a Sandra kurejea nchini akiwa yupo fiti.

Habari rasmi kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba, mama mzazi wa Diamond amerejea nchini wikiendi iliyopita huku hali yake ikionekana kuimarika vizuri tofauti na mwanzo ambapo alirejeshwa nchini akiwa hoi kufuatia kushambuliwa na ugonjwa wa kupooza mkono na mguu.

“Kwa taarifa yenu mama Diamond amerudi yupo nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar).
“Cha msingi anamshukuru Mungu kurejea kwa afya yake ambapo kwa sasa yupo fiti, kaondokana na tatizo la kupooza, kwa sasa anaweza kutembea na kushika chochote kwenye mkono.


“Nimefurahi sana kumuona kwenye hali hiyo maana sasa hata unapoongea naye mwenyewe unajisikia faraja kwani ana amani moyoni mwake, ingawa bado anamalizia kutumia dozi na mara kadhaa dawa anazokunywa zinamfanya kupitiwa na usingizi sana, ila kwa hali yake sasa hakuna ubishi tena amepona na familia ina amani kwa jumla,” kilisema chanzo chetu kinachomtembelea mama Diamond nyumbani mara kwa mara. Jirani wa mama huyo ambaye hakupenda jina lake kuandikwa alisema kitendo cha mama Diamond kurejea akiwa na afya njema kimemfurahisha sana.

No comments:

Post a Comment