INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, February 10, 2015

JADA IMEBAKIZA SIKU CHACHE KUINGIA DUKANI

Wapenzi wangu napenda kuwajulisha ya kuwa tumebakiza siku chache sana filamu yangu kuwa madukani. Ninamshukuru Mungu kwani kazi ya kuandaa filamu hii ilikuwa ngumu sana, lakini leo nina kila sababu ya kumshukuru Mungu, imeshamalizika na siku ya tarehe 19.02.2015 itakuwa sokoni.

Ninaamini ya kuwa hutanidondosha mdau wangu kwani tumetoka mbali mimi na wewe, na umekuwa ukiniunga mkono kwa kununua filamu zangu. Hata wewe ambaye ni mdau wangu mpya ninakuomba sana katika filamu hii ya JADA uzidi kuniunga mkono.

Mkurugenzi wa J-Film 4 Life Jeniffer Kyaka (Odama)

Najisikia faraja sana ninapoona wadau wangu wanaacha kazi zao na kuangalia kile ambacho nimekitunga kwaajili ya kuijenga jamii yetu ya Kitanzania. Katika filamu hii utaweza kuona ni jinsi gani mama wa kambo anavyodharauliwa na mtoto ambaye anamlea kutoka kwa mama mwingine na pia jinsi gani mwanaume anavyokuwa bega kwa bega na mwanae kumnyanyasa mama wa kambo. Filamu hii ni fundisho tosha sana kwa wale wote wanaopitia matatizo kama hayo.

Ninachokuomba kama mdau wangu, jaribu kuwasambazia na watu wengine ujumbe huu wa ujio wa filamu yangu ya JADA ili waweze kununua na kujifunza mengi kupitia filamu hii. Lengo langu ni kuona jamii ya inabadilika na kuwa na maadili mema. Filamu hii imetengezwa na kampuni yangu ya J-Film 4 Life iliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam

Nakushukuru sana mdau wangu. Tupo pamoja!!!

No comments:

Post a Comment