INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, July 30, 2012

BILA MILIONI TATU HUJAMPATA SHILOLE


 
Ikiwa ni tofauti na wasanii wengine, mwanamuziki na muigizaji huyu amejiwekea kiwango chake cha shoo pamoja na uigizaji kwamba yeye anapatikana kwa kiwango cha juu cha milioni tatu.

"Mimi ni msanii ambaye ninajiamini na kile ninachokifanya, kwakuwa naamini nipo katika soko kwa sasa, mimi hunipati bila milioni tatu, ingawaje naweza kupunguza lakini hicho ndio kiwango kinachofahamika" anasema Shilole.

Anaongeza kuwa licha ya shoo nono anazozipata, katika kalenda yake ameshakuwa na shoo kadhaa ambazo anatarajia kuzifanya hapo baadaye "mpaka sasa nina shoo zaidi ya tatu kwa wiki hivyo kwa mwezi ninapata shoo zaidi ya 12 na wakati mwingine zinabebana shoo mbili kwa siku moja" anafafanua muigizaji huyo.

Licha ya kazi anazozifanya msanii huyu ambazo zipo machoni mwa mashabiki wake, Shilole ni mjasiliamali ambaye anafanya kazi mbalimbali ikiwemo kumiliki duka la nguo lililopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni mwezi mtukufu wa ramadhani, Shilole hivi sasa amesimama kazi zingine na kwa sasa anauza duka na kurekodi kazi kazi zake za muziki mpaka hapo mfungo wa mwezi wa Ramadhani utakapokwisha.

"Katika kipindi hiki nipo bize na kazi zingine, kuna baadhi ya kazi zangu za ujasiriamali mbalimbali ambazo nimesimama kwa wakati huu, na sasa nauza duka na kazi za kurekodi za muziki na hivi karibuni watu watarajie kupata wimbo wangu mpya wa Dudu niliouimba nikiwa na Q Chief" anasema Shilole.

Shilole anasema katika maisha yake ana matarajio ya kuja kuwa msanii mkubwa na mwenye ubunifu kama ilivyo kwa wasanii wa nchi za ughaibuni.

"Unajua ukifika Hollywood unakutana na msanii ambaye ana fanya kazi zaidi ya moja, si kwamba anatumbukia tu ila kipaji kinazingatiwa zaidi na hivi ndivyo alivyo shilole" anajinadi huku akisisitiza kuwa sanaa pekee haitoshi katika maisha yake, ila ujasiriamali ndio nguzo anayoitegemea zaidi ili kuyafikia malengo yake.

Source: Vituko vya Mtaaa

No comments:

Post a Comment