INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, July 11, 2012

FILAMU YA SAYLA KWAAJILI YA KUMCHANGIA SAJUKI NA MKEWE WASTARA KUZINDULIWATarehe 13 Mwezi wa Saba, 2012 katika jiji la Arusha, filamu ya SAYLA itazinduliwa rasmi. Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii na watu maarufu takribani 27 ilirekodiwa maalum kwa ajili ya kuonyesha kuwa kwa kutumia sanaa, sisi watanzania tunaweza kusaidiana wakati wa matatizo.
Filamu hii maalum kwa ajili ya kuwasaidia Sajuki na Wastara waliokuwa katika wakati mgumu wa kutafuta pesa za matibabu, itazinduliwa kwenye ukumbi wa Naura Springs na kuhudhuriwa na watu wengi maarufu nchini akiwemo Mh Shyrose Bhanji na wabunge wengine wa Bunge la Afrika Mashariki, Wema Sepetu akiongoza kundi la wasanii wa Bongo Movie pamoja na wengine kama Snura, Shilole ambao watatumbuiza kwa kushirikiana na Ndege mnana Linah, kwa mara ya kwanza jijini Arusha toka adondoke.

SAYLA ni filamu ya kihistoria iliyoshirikisha idadi ya kubwa ya mastaa kuliko yeyote ile, itazinduliwa pamoja na video na behind the scene za nyimbo ya Mboni yangu!

Baadhi ya watu walioshiriki kwenye hiyo project ni kama ifuatavyo: Mh Zitto Kabwe, Mh January Makamba, Mh Halima Mdee, Mh Esther Bulaya, Mh Vicky Kamata, Mh Shyrose Bhanji, Mzee Chillo, Mzee Hashim Kambi, Muhogo Mchungu, Bi Kidude, Sharo Milionea, Mboto, Kitale, Wema Sepetu, Davina, Ephrahim Kibonde, Adam Mchomvu, Arnold Kayanda, George Goyayi, Mairmatha wa Jesse, Rose Chitala, Ruben Ndege, Irene Paul, Dully Sykes, Chege, Madee, Recho, Ommy Dimples, William Mtitu, Mwana FA na wengine wengi.

Filamu hiyo imetayarishwa na timu kubwa ya waandaji wakiwemo William Mtitu, Simon Mwakifamba, Zamaradi Mketema pamoja na Shamim (8020 blogspot.com).

Tusikose kwenye uzinduzi huu wa hadhi ya kimataifa ambapo kwa mara ya kwanza jijini Arusha, wageni watapita kwenye REd carpet maalum.

Kiingilio ni Shs 20,000/= na Shs 10,000/- viti vya kawaida. Na filamu inategemewa kuanza saa 3 kamili usiku katika ukumbi wa Naura Springs.

No comments:

Post a Comment