INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, July 4, 2012

WATUNZI WASIO NA UBUNIFU WANASHUSHA THAMANI YA FILAMU ZETU – AUNTY EZEKIEL…!!


MSANII nguli katika tasnia ya filamu bongo, Aunty Ezekiel, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa anaamini kukua au kuporomoka kwa tasnia hiyo kutatokakana na watunzi wenyewe pale wanapokuwa wanatoa stori zinazofanana bila kutumia ubunifu.

Mkali huyo alidai kuwa zipo baadhi ya filamu ambazo hakutaka kuzitaja majina ambazo zinafafa, na ndizo zinazoweza kuwafanya mashabiki pamoja na wadau kushindwa kuzitofautisha pindi zinapokuwa sokoni.

“Kufanana kwa filamu kunasababisha hata zinapokuwa sokoni watu washindwe kuzinunua kitu ambacho hata maisha ya wasanii yawe magumu kwani kazi zao huwa zinafanya vibaya sokoni,” Alisema Aunty.

No comments:

Post a Comment