INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, July 23, 2012

JENNIFER KYAKA (ODAMA) - NAWASHUKURU WOTE KWA MCHANGO WENU KUHUSIANA NA KIFO CHA MAMA YANGU MDOGO

Nawashukuru wote mliofika katika hospitali ya Ocean Road siku ya Jumapili kwaajili ya kumuaga mama yangu mdogo, aliyefariki siku ya Ijumaa katika hospitali ya Ocean Road - Dar es Salaam. Ninawashukuru sana tena sana, mmefanyika baraka kwangu na kunifariji sana katika kipindi hicho kigumu. Nimetambua kuwa kumbe nina ndugu na marafiki wanaonipenda katika ulimwengu huu.

Mungu wangu na awarudishie mara dufu kwa mchango wenu na muda wenu mlioupoteza kwa kuja kumuaga mama yangu mdogo, Ocean Road hospital. Pia nawashukuru wale wote waliopiga simu zao kunifariji na kunitia moyo. Wengine mlifika nyumbani kwangu kunifariji na kunipa mawazo ya jinsi gani mama yangu atasafirishwa kwenda Shinyanga kwaajili ya mazishi.

Jennifer Kyaka (Odama)

Ndugu zangu nawashukuru sana kwa wema wenu na upendo wenu mliouonyesha kwa mama yangu akiwa amelazwa pale  hospitalini. Nimeona huduma zenu, mmekuwa bega kwa bega kuhakikisha mama yangu anapewa yale mahitaji yaliyokuwa yanahitajika.

Nawashukuru madaktari wa hospitali ya Ocean Road kwa juhudi zenu. Mmetumia elimu yenu na ujuzi wenu kuhakikisha mama yangu mdogo anapona, lakini haikuwezekana kutokana na Mungu kumpenda zaidi.

Nawashukuru Watanzania wote kwa maombi yenu. Sina cha kuwalipa, ila Mungu wangu atawalipa. 
Ahsanteni sana na Mungu bariki familia zenu na kazi ya mikono yenu

AMENI

No comments:

Post a Comment