INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, July 23, 2012

KESI YA LULU KUPELEKWA MBELE NA MSAJILI MAHAKAMA KUUElizabeth Michael 'Lulu'

MSAJILI wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi Amiri Msumi ameahirisha kesi inayomkabili msanii wa maigizo nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini Steven Charles Kanumba Aprili 7 mwaka huu .

Akiahirisha kesi hiyo jana Msajili huyo Msumi alisema kutokana na sababu za Jaji anayesikiliza kesi hii katika Mahakama Kuu Jaji Dk. Fauz Twaib kutokuwepo Mahakamani amelazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 20.

"Kwakuwa Jaji Dk. Fauz Twaib ni mwalimu katika chuo cha Sheria hivyo yuko katika mitihani naahirisha kesi hii hadi tarehe hiyo niliyoitaja ambapo itakuwaja kwa kutajwa".

No comments:

Post a Comment