INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, July 13, 2012

MWIGIZAJI LATIFA KUINGIA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI




STAA wa filamu za Swahiliwood, Latifa Idabu Badra, ameamua kufungua kipaji chake kwa upande mwingine katika kuimba na tayari amefanikiwa kurekodi wimbo alioupa jina la 'Twende Sawa'.

Badra ameiambia Mwanaspoti kuwa yeye tangu awali alikuwa akiimba, lakini kutokana na mazingira ya kidini ya nyumbani kwao alishindwa kufanya hivyo mapema.

Toka kitambo nilikuwa nikiimba labda hata ningetoka katika uimbaji kabla hata ya filamu, lakini kutokana na wazazi wangu kuwa waswalina haikuwa rahisi," anatoboa siri.

"Muziki ninaoimba ni Hip Hop ambao unaonekana kama ni muziki wa kihuni, kwa sababu ni kitu ambacho ninacho rohoni kwangu sina budi kukifanya sasa."

Msanii hiyo anasema kuwa kuna wakati ambao watoto hupoteza vipaji vyao kwa sababu ya wazazi kushindwa kubaini uwezo na vipaji vya watoto husika, yeye anashukuru kuwa kwa sasa anaweza kufanya jambo lolote katika kuibua vipaji vyake kwani amekuwa ni mtu mwenye maamuzi yake ana maisha yake ambayo si tegemezi tena.

No comments:

Post a Comment