INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, July 23, 2012

MOVIE MPYA YA BATMAN YAZUIA KASHESHE


Filamu mpya ya Batman inayoitwa The Dark Knight Rises imeanza kuonyeshwa jana.Filamu hiyo ambayo imecchezwa na Christian Bale imeanza kuonyeshwa nchini Marekani jana katika kumbi mbali mbali za sinema.Watu wengi waliojitekeza katika Theater ya 16 century Colorado wamekumbwa na maafa baada ya mtu asiefahamika ukingia na kupiga risasi hovyo.Watu zaidi ya 12 wamepoteza maisha akiwemo mtoto wa miaka 12,70 wamejeruhiwa pia yumo mtoto wa miezi mitatu.


Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la James Holmes mwenye miaka 24.Aliingia ukumbini humo akiwa kavalia kama mmoja wa wahusika ambae amecheza kama adui katika filamu hiyo Tom Hardy aliyetumia jina la Bane.Anaonekana pichani.Alipoingia akatupa bomu la moshi na kisha kuanza kurusha risasi hovyo.

Wanafamilia mbali mbali wakifarijiana


Baba ambae mtoto wake wa miezi mitatu alipigwa risasi ya mgongoni akiwa hospital katika hali ya huzuni na kuchanganyikiwa.

Miongoni wa waliofariki yupo dada mtangazaji wa tv Jessica Ghawi.Muda wote akiwa katika jumba la sinema alikuwa akitweet namna anavyofurahia movie hiyo mpaka mauti yalipomkuta.

Tukio hilo limetokea jana usiku katika mji Colorado eneo linaitwa Aurora.Rais wa Marekani Barack Obama ametuma salamu zake za rambi rambi kwa wafiwa na kuwaomba wanachi wake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu.Pia akawaomba kuwaombea wakazi wa eneo hilo waweze kupita katika wakati huo ambao umewaacha katika mshituko.

No comments:

Post a Comment