Mke wa rais
Mama Salma Kikwete alijiunga na wafanyakazi wa kiwanda cha Sadolin Paint
(ambacho ndicho kilichozindua rangi bora ulimwenguni ya DULUX hapa Tanzania),
pamoja na wanajamii wote, wageni waheshimiwa, maofisa wa serikalini, waalikwa
wakijumuika na watoto wa kijiji cha SOS
Lengo kubwa
lilikuwa ni kupaka rangi za kung’ara na kubadilisha hali ya rangi iliyokuwa
ukungu na chafu.. Watoto hawakuishia kupaka rangi ya kuta bali walipaka na sura
zao. Kulikuwa na DJ na watoto walipata muda wa kuimba nyimbo zao.
Mama Salma
Kikwete alishirikiana katika shufghuli nzima ya upakaji rangi, kupanda mti wa
kumbukumbu na kuwashukuru waandaji.
Mkurugenzi
wa DULUX, Dr. Alex Lengeju alimshukuru Mama Salma Kikwete na muwakilishi
mwigizaji wa filamu Tanzania,
Jennifer Kyaka (Odama) kwa kazi nzima walioifanya na watoto wa kijiji cha SOS
Kituo cha
chekechea cha kijiji cha SOS ndicho kilichobahatika kuwa cha kwanza kupata
huduma hii.
NB: DULUX ni rangi murua ya Akzonobel na inapatikana katika nchi nyingi kama 26 na mabara kama Ulaya, Amerika Kaskazini, Latini Amerika, Asia na Afrika. Makao makuu yako Slough Uingereza
NB: DULUX ni rangi murua ya Akzonobel na inapatikana katika nchi nyingi kama 26 na mabara kama Ulaya, Amerika Kaskazini, Latini Amerika, Asia na Afrika. Makao makuu yako Slough Uingereza
Madhumuni
ya kampuni hii ni kubadilisha mazingira machafukwa rangi za kung’ara.
Kitu pia
kupanga kwa pamoja furaha na huzuni katika kufanya utofauti katika maisha ya
watoto.
Odama: akielekea Kijiji cha SOS
Leo ni leo rafiki yangu, Mama Salma Kikwete na Odama LIVE kijijini kwetu...Mbona tunabahati!!!!.
Hivi ni vyeti tunakupa mheshimiwa Nagu
Tulia nikupendezeshe, utapata zawadi kwa wageni wetu hapa kijijini
Mwana naomba utulie kabla ya kuanza kupaka rangi ukutani ngoja tuanze na nyinyi kwa usoni kama mfano.
Mwanangu lazima ufike mbali, Baba yako JK aliaanza hivi hivi..Kazana
Wall Painting ikiendelea na mama Salma Kikwete
Mheshimiwa Nagu akichekelea ucheshi wa Odama
Nashukuruni sana DULUX kwa zawadi yenu
No comments:
Post a Comment