INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, July 30, 2012

WEMA KUMRUDIA MAMA YAKE TENA!

KATIKA kukamilisha mfungo wake wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amekubali kupatanishwa na mama yake mzazi, Miriam Sepetu, hivyo kukamilisha usemi kuwa mtoto hakui kwa mzazi wake, Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Wema, baada ya staa huyo kutofautiana na mama yake kisa kikiwa ni mahojiano aliyofanya mzazi huyo runingani ambayo hayakumpendeza Wema, hivi karibuni wamekutanishwa na kurejesha amani iliyokuwa imetoweka kati yao.

“Mimi najua undani wa ishu nzima, tangu yale mahojiano na nyiye (Global) mkaandika kuwa mama Wema alimtia aibu mwanaye, hali ilikuwa mbaya hadi juzi walipopatanishwa ndiyo wamerudisha ushosti wao,” kilisema chanzo hicho.


WAZEE WAWAPATANISHA

Chanzo chetu kilidadavua kuwa pamoja na Wema kwenda kumwangukia mama’ke, kuna wazee ambao walitinga nyumbani kwa Wema, Kijitonyama ‘Hollywood’, Dar waliotoka upande wa mzazi huyo ambao walikwenda kumsihi afanye hivyo.

“Hazikuwa jitihada zake peke yake za kutaka kumaliza tofauti kati yake na mama’ke bali wale wazee takriban wanne walizungumza na Wema na kumwelekeza namna ya kumaliza tofauti zake na mzaa chema huyo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Hao wazee ndiyo waliwakutanisha kwa mama Wema, Sinza-Mori, Dar na kumaliza chokochoko zote na sasa Wema na mama’ke mambo ni ‘mswaano’.


HALI ILIKUWA MBAYA SANA
Chanzo hicho kiliendelea kushusha data kuwa kulikuwa na ulazima wa Wema kutinga kwa mama’ke na kumwangukia kwani suala hilo lilikuwa likimpasua kichwa na kusababisha hali kuwa mbaya kati ya wawili hao kwa sababu hakukuwa hata na salamu.


WEMA ASHINDA KWA MAMA’KE
Baada ya kusikiliza maelezo hayo kutoka kwa chanzo, Julai 23, mwaka huu saa 5 na sekunde 35 asubuhi, Ijumaa lilizungumza na Wema kutaka kujua alikuwa wapi wakati huo ambapo alijibu kuwa anaenda kwa dada yake kumchukua mtoto aliyemtaja kwa jina la Sasha kisha kwenda kushinda naye Sinza-Mori kwa mama yake.

Alipoulizwa kama ni kweli kuna wazee walimfuata na kumpatanisha na mama yake, staa huyo wa muvi ya Super Star itakayoingia sokoni Agosti alikiri kutokea kwa suala hilo.


HUKO NYUMA
Wiki kadhaa zilizopita, Wema na mama yake walitibuana baada ya mzazi huyo kuwatemea mbovu mashosti wa mwigizaji huyo alipokuwa akihojiwa runingani.

No comments:

Post a Comment