INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, July 23, 2012

PASTOR MYAMBA WA BONGO MOVIE AFUNGUKA KATIKA KITUO CHA PRAISE POWER RADIO

Haya yalikuwa mazungumzo kati ya mtangazaji wa Praise Power, James Temu ambaye na yeye ni mwigizaji wa filamu za Kitanzana na Pastor Myamba Supar Star wa Bongo Movie .

James Temu (Uncle Jimmy) alisema:-

Kupitia kipindi cha Rise & Shine ni nacho fanya mimi na Swahiba yangu Erick Martin kuanzia Saa 6:00 adi Saa 10:00 asubuhi, Pastor Myamba Supar Star wa Bongo Movie amesema Filamu zote anazo fanya kupitia Kampuni yake zina asilimia 80% za kuwawaleta watu kwa Yesu.

Amefunguka zaidi na kusema huu ni mwaka wake kuakikisha analiteka soko la filamu nakulipeleka sehemu nyingine ya watu kufahamu umuhimu wakuijua siri iliyo kwenye Wokovu.


Uncle Jimmy na Myamba kwenye One end 2 Praise Power Fm

Pastor Myamba ambae alichelewa kufika katika kipindi siku ya ijumaa kutokana na foleni za hapa Bongo amesema Filamu yake mpya ya {GOD"S KINGDOM} aliyofanya na Kampuni yake ya Born Again Films Production. Ni Filamu inayoonyesha kazi ya Kristo katika kuwaleta watu kwake, Ni filamu iliyokuwa na upako wa ajabu kwa maana baadhi ya sehemu walizokuwa wakifanya shooting ilibidi kusimamisha ili Roho mtakatifu afanye kazi yake.

NUKUU-"Uncle Filamu hii nilimuona Mungu akiwaudumia watu kwa namna ya ajabu,kuna kipindi watu walipandisha Mapepo kweli ikabidi nichukue jukumu lakuanza kuwaombea.Yani sasa sio filamu tena bali ilikuwa Uduma.Mwisho wa Nukuu".

Wiki ijayo ya Tarehe 27/7/2012 Pastor Myamba atakuja kuendeleza muendelezo wa Topic yetu ya (Nini faida ya Filamu za Kitanzania katika Maisha ya Mtu alie okoka.Je? Filamu hizi zinaweza badilisha maisha ya Mtu asie jua wokovu)


Pastor Myamba na Joyce Charz rafiki yako wa karibu akijishebeda na Myamba.

Usikose Rise$Shine ya Ijumaa itakapo fika Saa 9:00 asubuhi nitakapo kuwa na gwiji la Filam Emmanuel Myamba a.k.a Pastor Myamba atakapo funguka kwa undani.

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget