INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, July 17, 2012

HIZI NDIO KAULI ZA WEMA SEPETU, FRANCIS CHEKA NA MASANJA MKANDAMIZAJI KUHUSU KUWEKA MAJINA BADALA YA NAMBA KWENYE MAGARI YAO.

Sote tunafaham kwamba Serikali imeruhusu watanzania wenye uwezo wa kulipa milioni tano kwa miaka mitatu ili kuweka majina kwenye magari yao badala ya namba za kawaida wafanye hivyo.

Kwa sababu kwa kiwango kikubwa kwenye nchi nyingine mastaa ndio huwa wanaandika majina yao kwenye magari, nimeanza kuwauliza mastaa kadhaa wa bongo.

Movie star Wema Sepetu amekua wa kwanza kulijibu swali langu kwa kusema “sitotaka kufanya hivyo, wale wanaotaka kuuza watafanya hivyo mi sio mtu wa kuuza bwana, tayari nina gari zaidi ya moja lakini sitopenda kufanya hivyo kwenye gari langu lolote, kwa nini kila mtu nikipita aone Wema yule pale….? napenda magari yangu jinsi yalivyo na namba hizo hizo zinatosha.

Bondia Francis Cheka amesema “naweza kufanya hivyo kwa sababu jina langu ni jina ambalo watu wengi wanalifahamu na ni rahisi kufanya hivyo, ni kitu kizuri”Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi amesema “kama ulimuhoji staa akasema ataandika lile jina kwenye gari yake yani huyo ni anaiga tu tuliotakiwa kufanya hivyo ni sisi tuliookoka kwa sababu kwenye biblia tunaambiwa vyovyote Mungu anavyokubariki simama kutoa ushuhuda, mimi niko tayari kufanya hivyo hata sasa hivi kwa sababu Account zangu, si unaona ndugu Millard nikitembea hivi pochi imetuna, sio imetuna pesa… ni kadi za benki”
Moja ya magari ya Wema Sepetu.
Hili ni gari la Jose Chameleone wa Uganda, magari yake yote kayaandika DOCTOR kwenye namba.


Hili ni gari la mwanasoka Mkenya Mariga.

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget