INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, July 25, 2012

MWIGIZAJI WA BONGO MOVIE- JACQUILINE WOLPER AWAFURAHISHA WAHEHE WA IRINGA

MWANADADA nyota katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, Jaqueline Masawe Wolper, Jack Wolper, hivi karibuni alikuwa kivutio mjini Iringa kutokana na kuvaa gauni la heshima mithili ya mtawa

J Wolper

Watu wanaomfahamu msanii huyo, hawakuamini kuwa aliyevaa gauni hilo alikuwa Wolper ambaye mara nyingi huvaa nguo za kutatanisha na kujiachia.

Lakini siku hiyo alionekana kama mtawa au mama wa familia asiye na makuu.
Alikuwa katika Uwanja wa Samora mjini Iringa wakati wa uzinduzi wa muziki wa Injili kutoka kwa msanii Masanja Mkandamizaji.
"Ninajua kuwa mimi ni nyota kwa sasa, najaribu kwenda na matukio katika uvaaji wangu, siwezi kuvaa vazi la Disko au kuigizia katika sehemu inayohubiriwa neno la Mungu," alisema msanii huyo hukun akitabasamu.


Wolper (kulia) akiwa katika uzinduzi wa Masanja Iringa

"Ningefanya hivyo hapa, ningekuwa nashiriki kusikiliza neno la Injili au naigiza? Nipo kwenye uzinduzi wa albamu ya Masanja Mkandamizaji ambaye ni msanii mwenzetu nasi tumekuja kumsindikiza katika kazi ya kumtukuza Mungu.

"Nami namtukuza Mungu hata katika kuvaa kama unavyoniona nikiwa katika gauni safi tena la kiheshima."

Watu waliofika katika uwanja huo walishindwa kujizuia na kuanza kumsifia kwa nguo aliyovaa hata nywele zake alivyoziweka, hazikuwa za utata.

No comments:

Post a Comment