INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, August 29, 2012

BABY MADAHA NA ISABELA WANASWA TENA

MATUKIO ‘hot’ ya wasanii wawili Bongo, mwigizaji ambaye pia ni mwana-Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha na chipukizi wa filamu, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ yamedhihirisha wao ni sikio la kufa,
Hivi karibuni, Baby Madaha alinaswa na kamera yetu kwa mara nyingine tena akiwa hajitambui kwa kulewa chakari kwenye Baa ya Uhuru Peak, Kinondoni jijini Dar ikiwa ni mara ya ishirini kwa kipindi kifupi kukutwa katika hali hiyo.
Baby Madaha alipoulizwa kwa nini anapiga ulabu hadi anazima tena mbele ya meneja wake, Mercey Kayuni, alidai ni maisha yake binafsi hivyo aachwe na maisha yake.
Wakati Baby Madaha akishauriwa kuacha ulevi kwani utampeleka pabaya, katika misele ya Ijumaa Wikienda akanaswa Isabela kwenye Ukumbi wa Dar West, Tabata jijini Dar kwa mara nyingine akifanya uchafu hadharani, yaani mambo ya chumbani akiwa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Bonny.
Isabela alipobanwa kuhusu kujilegeza kwa midume hakuwa na la kusema zaidi ya kuonekana kutojielewa.

No comments:

Post a Comment