INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, August 29, 2012

GENEVIEVE ARINGISHIA PETE YA UCHUMBA; KUFUNGA NDOA HIVI KARIBUNI?Muigizaji wa kike mwenye mafanikio na anayetafutwa zaidi na watayarishaji wa filamu nchini Nigeria, Genevieve Nnaji huenda hivi karibuni akavaa shela ya harusi na kusema ‘I DO’.
Ripoti kutoka nchini Nigeria, zimesema kuwa muigizaji huyo na mama wa mtoto mmoja ameshachumbiwa na amekuwa akijionesha kwa watu kuwa muda si mrefu atakuwa mke wa mtu.
Kwenye akaunti yake ya twitter hivi karibuni aliweka picha inayomwonesha akiwa na pete ya uchumba na kuandika maneno yasemayo “kisses especially for U”
Kutokana na picha hiyo, mitandao mingi ya Nigeria imehitimisha kwa kusema kuwa tayari amechumbiwa.
Baadaye Genevieve aliandika kufafanua kuhusu picha hiyo iliyopo kwenye mtandao wa Instagram akisema, “I wear that ring on my right so people won’t think anything of it. But I guess I’m on my own there. Lol!!”

No comments:

Post a Comment