STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ anadaiwa kubondwa na mwanaume mmoja mwigizaji aitwaye Mandela Nicholaus a.k.a Jacob, hivyo kulazimika kukimbilia Kituo cha Polisi cha Pangani, Ilala jijini Dar es Salaam kuokoa maisha yake,
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilichokuwa eneo la tukio, sakata hilo la aina yake lilitokea kwenye Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Jack Chuz na waigizaji wenzake walikuwa wameweka kambi kwa ajili ya kurekodi filamu.
Chanzo hicho kilidai kuwa Jacob alimuuzia Jack Chuz muswada wa filamu (script) na kukubaliana kuwa ataiongoza lakini kabla ya kumaliza kazi hiyo, muongozaji huyo alidai kuwa waigizaji aliokuwa akiwaongoza walikuwa wakimfanyia dharau hivyo kusitisha zoezi hilo.
Chanzo hicho kilitiririka kuwa baada ya kusitisha zoezi hilo, Jacob alimtaka Jack Chuz amrudishie chake kwani alikuwa amempatia Sh. milioni 1.4 lakini sistaduu huyo alisema hawezi kumpa fedha hizo ndipo likaibuka varangati zito hotelini hapo.
Ilisemekana kuwa mtiti huo ulitawaliwa na ngumi na mateke ya judo, hali iliyosababisha kuibuka kwa mayowe na vilio vya kuomba msaada kabla ya baadhi ya wasanii waliokuwa na Jack Chuz, Slim Omary, Mary Mtema na mpiga picha wao, Mohammed Kibinda kumnasua staa huyo ambaye alitoka nduki hadi Kituo cha Polisi cha Pangani, Ilala na kufungua jalada la kesi namba ILA/RB/3042/12 -SHAMBULIO.
lilifika kituoni hapo na kuwakuta wawili hao ambapo Jacob alisema anamdai Jack Chuz Sh. milioni 1.4 kwa ajili ya kumuuzia script ya filamu hiyo pamoja na kumuongozea kabla ya kutokea mtafaruku.
Kwa upande wake, Jack Chuz aliliambia kuwa anachoweza kumlipa ni shilingi laki tano na si zaidi ya hapo kwa kuwa ‘dairekta’ huyo alitaka kumkomoa kwani hamdai kiasi hicho.
Paparazi wetu aliwaacha wawili hao wakiwa kwenye harakati za kutaka kuburuzana kortini.