INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, August 16, 2012

NORA AWABWATUKIA MASTAA WA KIKE BONGONuru Nassoro ‘Nora

’MSANII wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amewabwatukia wasanii wa kike wanaoendekeza tamaa ya fedha na kuharibu tasnia nzima ya uigizaji.

Akichezesha taya na Tollywood Newz hivi karibuni, Nora alisema anaumizwa sana na wasanii ambao hawana msimamo wanaofanya sanaa ya uigizaji kuwa ni sehemu ya kuuzia sura jambo ambalo linaweza kuifanya hata serikali kushindwa kuisaidia sanaa hiyo kutokana na skendo za mara kwa mara zinazowakumba wasanii.

Aidha, alisema wasanii wa kike wanatakiwa kujitambua na kuachana na kujichanganya na mambo yanayowaharibia sifa katika jamii kwani wana nafasi kubwa ya kuitangaza sanaa nje ya nchi kama ilivyofanywa na marehemu, Steven Kanumba.

“Huwa inaniuma sana kuona wasanii wa kike wanavyokuwa na skendo nyingi kuliko kufanya kazi, kwa nini wasiachane na mambo hayo ya hovyo na kujikita katika kazi?

“Lakini kwa upande mwingine hata waandaaji wa filamu wanachangia kwani wakimuona msichana ana sura nzuri au umbile zuri wanamchukua hawajui kwamba kuigiza ni kipaji, matokeo yake ndiyo haya, wanafanya uigizaji ni sehemu ya kuuza sura”, alisema Nora.

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget