INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, August 16, 2012

SINTAH NA AGNESS MASOGANGE WAMESAMEHEANA

Lile Bifu baridi lilikuwa linafukuta likiwahusisha nyota wawili wa kike wanaofanya vizuri kupitia filamu na muziki hapa Bongo Christina Manongi 'Sintah' na Agness Gerald 'Masogange' limezikwa rasmi kufuatia wawili hao kuombana msamaha

Katika mazungumzo ya dakika chache aliyoyafanya kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Sintah amearifu kuwa Agness alimpigia simu na kuomba msamaha na sasa ugomvi kati yao hamna tena na wanazungumza kawaida kama walivyo marafiki wengine.

"Sipendi uchonganishi jamani?? huyu dada alishaniomba msamaha na mimi na yeye tunaongea vizuri,,kama mtu anawashwa na yake aandike uchafu wake kupitia mitandao na ataona kitakachomkuta" alisema Sintah na kuandika pia kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii.

Akiendelea zaidi Sintah aliwataka watu waliokuwa wanamzungumzia mabaya kwa Agness waache kwani shoga yake huyo wa sasa kamwambia yote kuhusu watu hao ila ameamua kuwanyamazia na kuwaangalia tu.

"mimi simjui Agnes ila nikiona mtu kafanya makosa namsahihisha ndo mana alikuja kuniomba msamaha na sina kinyongo naye tena na maisha yanaendelea kama kawa" alisema Sintah.

"Nimemsamehe sasa maneno mengine mnayatoa wapi? kama mtu ana picha zangu za ngono zitoeni jamani kwanini mnanitishia??haaaaa nimeshatoka huko kitambooo sana lolest,,labda mtengeneze na za kutengeneza tunazijua hivihivi mtasubiri sana tena sana ninajiamini 100%.

Agnes alinieleza mkanda mzima wa yaliyomtokea na nikaona wasichana wanadhalilishwa sana wakipewa pombe""Jamani yale maisha ya twendeni tukamnywe mbona yamepita? so msiendelezee maneno yenu ya ajabu mimi na Agnes tunaongea tena siku ile ile ndo maana nilifuta posts na nimemsema sana nadhani ameanza kunisikiliza na akinisikiliza atafika mbali maana ni binti mzuri so mnaopenda watu wagombane poyeeeeeee"

,, mmeshushukaje??tafuteni mwingine kwangu ni fulllll stooooooop,, Agnes nakwambia hapa mbele ya watu huna marafiki ni wanafiki wao ndio wamenitumia video kwa mda wako uje nikuonyeshe waumbuke "
Sintah

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget