INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, August 14, 2012

MJUE BLANDINA CHANGULA(JOHARI)


Blandina Changula (amezaliwa tar. 27 Julai, 1983 mkoani Shinyanga, Tanzania.
 
Ni muigizaji wa vipindi vya telesheni na filamu nchini Tanzania.

Maisha ya Mwanzo

Blandina alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya sekondari ya kutwa ya Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.

Akiwa kidato cha pili alihamishiwa katika shule ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo huo baada ya kuingia kidato cha tatu akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam katika shule ya Greens iliyokuwa maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungo shule ambayo alimalizia kidato cha nne mnamo mwaka 2001.

Blandina Changula anatokea kundi la Kaole Sanaa Group, ni kundi ambalo Show alllinafahamika sana nchini Tanzania kwa kutoa nyota wengi wa uigizaji, Blandina nae ni mmoja kati ya nyota hao, wengine ni Steven Kanumba, Vincent Kigosi ( Mr Ray ), Tea na wengine wengi tu kutoka Kaole Sanaa Group

Hadi sasa ameishatoa filamu nyingi,pia ni mmiliki wa kampuni ya kutengeneza filamu ya RJ COMPANY.

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget