INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, August 25, 2012

FIESTA 2012: BONGO MOVIE STARS WAVAMIA MOSHI-TANZANIA



Mastaa wetu wa filamu hapa nchini, wametokelezeaje sasaaa


Wema Sepetu akijiweka sawa.


Wema Sepetu pia akizungumzia ujio wao ndani ya mji wa Moshi, kuwa wao kama Wasanii Nyota wa Filamu wamewasili mkoani humo kusaka vipaji vipya mbalimbali vya filamu, usahili huo unafanyika kwenye ukumbi wa Mr Price, ulioko mtaa wa Malindi.


Mmoja wa wasanii mahiri katika fani ya uigizaji hapa nchini, Wema Sepetu akifanya mahojiano mafupi na Millard Ayo wa Clouds FM mapema leo kwenye amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta ambalo linafanyika jioni ya leo mpaka lyamba ndani ya uwanja wa chuo cha Ushirika,ndani ya mji wa Moshi, ambapo katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni nusu mnyama tu a.k.a 5,000/= kwa kila kichwa.


Msanii mwingine nyota katika tasnia ya filamu, Aunt Ezekiel akielezea ni namna tamasha la Serengeti Fiesta lilivyowambamba wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake, na pia ujio wao kuwatafuta wasanii wapya chipukizi katika tasnia hiyo ambayo imekuwa ikikua siku hadi siku.




Millard Ayo akifanya mahojiano na Ray a.k.a Vincent Kigosi kuhusiana na ujio wao ndani ya mji wa Moshi


Jacob Steven a.k.a Steven akifafanua jambo mapema leo mtaa wa Malindi kuhusiana na suala zima la wasanii hao kulivamia jiji la Moshi.



Wema na Steve Nyerere Wakiwa katika mazungumzo yao ya hapa na pale.

Kiongozi wa msafara wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, Mully B akiwa na mastaa wa filamu, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel afu fulllll BBM kama kawa.


Wema Sepetu katika pozi na washabiki wake mapema mchana huu.

Pichani ni Gari aina ya Vits itakayotolewa jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, kwa mshindi atakaejishindia kwenye droo itakayofanyika katika uwanja wa chuo cha ushirika, ambako tamasha hilo litarindima mpaka majogoo.

Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo akiwa Live mapema leo mtaa wa Malindi katika mpango mzima wa amsha amsha kwa wakazi wa Moshi kuhusiana na tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ambapo pia katika tamasha hilo kutatolewa zawadi mbalimbali ikiwemo gari ndogo aina ya Vits kama uinavyo pichani ikinadiwa vilivyo.


Kawa kawa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta pia linatoa mafuta kwa magari daladala,pikipiki sambamba na baji lita 10 ama tano kutoka kampuni ya GAPCO ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo.

Wasanii machachari Bongo Move Wema Sepetu (kushoto) na Aunt Ezekiel wakicheza muziki wa bongo Fleva uliokuwa ukishushwa na Msanii wa Bongofleva,Ferooz katika uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Bhaaaaass! katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi usiku huu. Tamasha hilo limebamba ile mbaya.

Ferooz akiwa na mmoja wa mashabiki wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.

Sehemu ya wakazi wa mji wa Moshi wakiendelea kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wanaotumbuiza usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Prezoo akiwarusha mashabiki kibao (hawapo pichani) waliojitokeza jioni ya leo kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012


Pichani juu na chini ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya na mmoja wa shiriki wa shindano la Big Brother Stargame,CMB Prezoo akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa chuo cha ushirika mjini Moshi.

Mmoja wa wasanii wa hip hop Joh Makini akikamua vilivyo usiku huu mbele ya umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwenye uzinduzi wa tamasha la Fiesta.

Msanii mahiri wa bongofleva,Lina akiwa na densaz wake wakilishambulia jukwaa vilivyo.

Lina akiimba wimbo wake Yalaiti

Mkali mwingine wa hip hop Mwana FA akishusha mitindo huru.

Pichani juu na chini Mwana FA akilishambulia jukwaa vilivyo kwa mitindo yake huru iliyokuna vilivyo mashabiki wake,waliofika kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.


Wasanii wa nyota wa Filamu hapa nchini nao walijumuika kwa pamoja kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani jukwaani ni Wema Sepetu,Jacob Steven a.k.a JB,pamoja na Aunt Ezekiel wakilisakata sebene.

Ray nae akilisakata sebene vilivyo.





No comments:

Post a Comment