INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, August 9, 2012

MPOKI AMCHANA COP, "NENDA KWANZA FIELD"




Kwenye YOU HEARD ya XXL ya Clouds Fm, Soudy Brown amempigia simu Mpoki kumuuliza kuhusiana na story iliyoandikwa na gazeti la Ijumaa Wikienda kuhusiana na Masanja Mkandamizaji mwishoni mwa wiki iliyopita kudaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.

Katika mahojiano hayo Mpoki amemwambia Gossip Cop kuwa hana taarifa zozote kuwa Masanja amelazwa kutokana na kichapo hicho na kummshauri kuwa aende kwanza field ili ajifunze uandishi wa habari kwakuwa hauwezi.

Mpoki amejinadi kuwa yupo kwenye game kwa miaka 12 hivyo hayumbishwi na kitu.

Habari hiyo iliandikwa:

MCHEKESHAJI wa Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, mwishoni mwa wiki iliyopita anadaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea kwenye njiapanda ya Chalinze mkoani Pwani ambapo msanii huyo alikuwa akitokea Dar kuelekea Tanga huku akiendesha gari kwa kasi ya ajabu.

Chanzo hicho cha Ijumaa Wikenda kinachopiga kambi maeneo hayo kilieleza kuwa jamaa huyo alikutwa na kasheshe hilo baada ya ‘kuliovateki’ gari hilo lililokuwa likisindikizwa na polisi ambapo pamoja na kuzuiwa na wajeda hao, Masanja alijitoa fahamu na kujifanya kichwa ngumu.

Kilisema: “Baada ya ‘kuwaovateki’ wale polisi, ndipo nao (askari) wakamkimbiza hadi wakamkamata na alipotaka kuleta ‘mbovumbovu’ za kujifanya staa kama wale wenzake waliopoteza umaarufu na mvuto, ndipo akala mbata zake safi na soo likahamia kwenye Kituo cha Polisi cha Chalinze Njiapanda na kumshikilia kwa muda kisha kumuachia baada ya mahojiano.”
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Masanja ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kukamatwa na askari kutokana na makosa ya barabarani kwake ni suala la kawaida huku akikanusha kupewa kibano.

No comments:

Post a Comment