KUNA madai kwamba ule ‘mkoko’ wa kifahari wa staa wa maigizo Bongo, Jacqueline Wolper aina ya BMW X6 lenye Namba za Usajili T574 BXF linatarajiwa kuingizwa sokoni wakati wowote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya muda aliopewa nyota huyo kulipia deni lake la kukwepa ushuru wa shilingi milioni 70 kupita bila mwenyewe kusema chochote.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ‘mchuma’ huo ambao ‘umetaitiwa’ na Kampuni ya Udalali ya Majembe ya jijini Dar es Salaam kwenye yadi yao ya Mikocheni, umekuwa ukipata wateja kila kukicha ambao wanakwenda kuulizia siku ya mnada.Chanzo kingine kilisema kuwa mbali na wateja kumiminika yadi ya Majembe, kumekuwa na usumbufu mwingi kwenye ofisi za TRA, Posta jijini Dar ambapo baadhi ya matajiri nao wamekuwa wakilifukuzia gari hilo kwa lengo la kulinunua.“Tunashangaa sana, watu na fedha zao wanakuja hapa kulitaka gari la Wolper, mbona kuna magari mengi yapo toka mwaka juzi (2009) hawaji kuyanunua au kwa sababu hili ni la supastaa wa Bongo?” alihoji mfanyakazi mmoja wa TRA akiomba jina lake lisitajwe .
Akaongeza: “Unajua tatizo liko wapi? Baadhi ya wafanyakazi wa TRA nao wamekaa mkao wa kusubiri siku ya kutajwa kwa tarehe ya kulipiga mnada gari hilo ili wasuke mipango ya kupata cha juu kutoka kwa matajiri watakawaopigia debe na kushinda,” kilisema chanzo.
Amani lilipoongea na Wolper kuhusu gari lake hilo likitaka kujua nini kitatokea kama hatalikomboa kwa siku alizopewa na TRA ambazo zimepita, alijibu hivi:
“Kisheria gari linatakiwa likombolewe ndani ya miezi mitatu lakini mimi niliandikisha kuwa kwa mwezi mmoja nitakuwa tayari nimemaliza kila kitu. Hata hivyo, kimsingi na mimi nilimfikisha polisi Ndama Mtoto wa Ng’ombe ambaye alisimamia ununuzi wake mwanzo hadi mwisho. Kwa hiyo kama ni kukwepa ushuru ni yeye.
Gari la Wolper lilikamatwa Juni 28, 2012 kwa madai ya kukwepa ushuru, hadi Agosti 28, mwaka huu litakuwa limefikisha miezi mitatu ambayo ni ya kisheria lakini mwezi mmoja aliotaka Wolper uliisha Julai 28, 2012 hivyo kutoa fursa kwa TRA kutangaza siku ya kulipiga bei.
Wolper alilinunua gari hilo kwa shilingi milioni 250 za Kitanzania likiwa na sifa nyingi tofauti na magari mengine.
No comments:
Post a Comment