INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Sunday, August 19, 2012

“WIVU WA WANAUME NDIYO UNAONIFANYA NISIOLEWE MAPEMA” – SHILOLE…!!


MSANII anayefanya vizuri kwenye muziki kwa sasa ‘Shilole’, ameSEMA kuwa baada ya kuachana na mume wake kitambo amekuwa akitafuta mwanaume mwingine wa kumuoa lakini kila anayempata anakuwa na wa wivu kupiliza na ndiyo sababu inayomfanya aendelee kuishi mwenyewe kwani haitaji maisha ya kubanwa kama mtoto mdogo.

Shilole kwa sasa anatamba na ngoma yake inachokwenda kwa jina la ‘Dudu’, aliyokiachia hivi karibuni, ambapo
ndani ya ngoma hiyo anaongelea maisha ya ndoa.

Kauli ya msanii huyo, ilikuja baada ya kuzungumza na mwandishi aliyetaka kujua baada ya kuachana na mume wake
kitambo sasa anafanya mchakato gani utakaomuondoa kwenye upweke, ambapo alidai kila mwanaume anayempata amekuwa na wivu wa kupiliza kwani anaamini wakifunga ndoa wivu unaweza kupiliza zaidi.

“Yani mwanaume sijafunga naye ndoa tumekuwa wapenzi tu analeta wivu kiasi kwamba nikiwa kwenye himaya yake si itakuwa balaa, yani hapo tu ndiyo nachoka na suala la kuolewa kwani mi sitaki maisha ya kufugwa kama kuku,” alisema.

Hata hivyo kutokana na ishu hiyo ya kutoka na wanaume wengi ili kujua nani mwenye mapenzi ya dhati kunamfanya aonekane hajatulia lakini anaamini lengo lake ni kupata mwaume mwenye mapenzi ya dhati ingawa kila anayempata si yule anayetarajia.

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget