INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, August 29, 2012

BLOGU YA VITUKO VYA MTAA YAFUNGUKA KUMZUNGUMZIA ODAMA

Source: http://vitukovyamtaa.blogspot.com/2012/08/mfahamu-jennifer-kyakaodama.html

MFAHAMU JENNIFER KYAKA(ODAMA)

 
Jina Kamili: Jennifer Kyaka
A.k.a: Odama
Fani : Uigizaji
Kuzaliwa: 1983
Alikozaliwa: Bugando, Mwanza
Umri: 29
Makazi: Kinondoni - Biafra, Dar
Ndoa: Hajaolewa
STAA hot cake katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ ametokelezea kunako Hot 2 Hot na kuweka plain kuwa katika mafanikio aliyoyapata hakuna mkono wa mwanaume kama ilivyo kwa wasichana wengine mastaa wa mjini.
Odama alitiririka kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii na kile anachokipata ndicho anachofanyia mambo yote ya maendeleo ambapo hadi unaposoma hapa, anamiliki kampuni yake ya filamu ya J-Film For Life, magari mawili na mjengo.
“Mafanikio yangu yametokana na kazi zangu mwenyewe na hakuna mkono wa mwanaume, sitaki iwe hivyo ‘coz’ ndiyo maisha niliyoyachagua ya kutomtegemea mtu kwani kile ninachokipata kwenye filamu zangu ndicho kinachonipa maendeleo haya,” alisema Odama.
Hata hivyo, mwanadashosti huyo alisema kwa sasa ana mchumba na anatarajia kufunga ndoa mwakani.

No comments:

Post a Comment