INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, August 16, 2012

PENINA :'SIPENDI MAMBO YANGU YAONGELEWE HADHARANI'MSANII wa kike katika tasnia ya filamu Jennifer Raymond ‘Penina’ amelalamika kwa baadhi ya watu kuhusisha familia yake na mambo yake ya uigizaji au usanii kwa ujumla.

Msanii huyo aliyasema hayo baada ya kuulizwa kuwa ameolewa na ana watoto wangapi? Penina aliruka kwa kusema kuwa hawezi kuhusisha familia yake na Sanaa.“Mimi ni mke wa mtu, kwa maana nimeolewa lakini sipendi mambo ya familia yangu yasihusishwe na kazi yangu ya uigizaji kwa hiyo sipendi kuongelea mambo ya ndani huo ni utaratibu ambao tumejipangia na mume wangu kwa hiyo
siwezi kumtaja jina mume wangu wala kusema kama nina watoto wangapi?

Hayo ni mambo yangu binafsi siwezi
kuyaongelea hadharani,”anasema Penina.

Aidha msanii huyo alizidi kwenda mbele zaidi katika suala hilo la kuficha maisha yake na familia akitaka kutenganisha
na fani yake ya uigizaji na familia yake pale aliposema kuwa mumewe hataki kabisa ajulikane na jamii zaidi ya Penina
kujielezea yeye binafsi na si familia yake hatua hiyo ilikuja baada kuzuka tetesi kuwa msanii huyo ana mahusiano na
msanii wa muziki wa dansi fulani jina tunahifadhi Penina alikanusha.

“Habari hizo si kweli sina mahusiano na msanii huyo ni mtu ninayemjua lakini sipo naye karibu wala sina mazoea naye ila tu najua kuwa ni mwanamuziki na msanii mwenzagu kama mimi hakuna zaidi ya hapo, watu waongelee maendeleo si maisha ya watu,”anasema Penina.

Jina la msanii huyo lilitokana na filamu aliyoigiza na marehemu Kanumba, Penina kaigiza filamu nyingi sana
anazozikumbuka ni Last of money, Mirray kosa langu, Wema, Temptation, Kesi ya jinai, Penina, mateso ya moyo na
nyingine nyingi.

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget